Thursday, November 18, 2010

Shirika la Green Belt Movement




UKIZUNGUMZIA suala la uhifadhi na utunzaji wa mazingira,hautakuwa umetenda haki iwapo hutalitaja Shirika la Kimataifa la Green Belt Movement lililoanzishwa nchini Kenya mnamo mwaka 1977 chini ya mwasisi wake, Profesa Wangari Maathai.

Shirika hilo lenye sura mbili,moja ya kimataifa na ile ya kitaifa nchini Kenya limeundwa kama moja ya mashirika ya wanawake ya kiraia, ambalo limelenga katika kutetea haki za binadamu na kusaidia utawala bora na demokrasia ya mabadiliko ya amani kwa njia ya ulinzi wa mazingira duniani kwa ujumla.


Katika taarifa zake kuhusiana na shirika hilo,mwasisi huyo Profesa Maathai amesema lengo la kuundwa kwa shirika hilo ni kuziwezesha jamii duniani kote na kulinda mazingira na kukuza utawala bora na utamaduni wa amani baina ya kizazi kimoja na vijavyo.(Picha kwa hisani ya mtandao wa Green Belt Movement)

No comments:

Post a Comment