Thursday, November 18, 2010

Ghailani aingia matatani





MTANZANIA Ahmed Khalfan Ghailani aliyekuwa akikabiliwa mashtaka 281 yakiwemo ya mauaji katika mashambulizi ya kundi la kigaidi la Al Qaeda, dhidi ya ubalozi wa Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998,amepatikana na hatia ya kula njama na kushiriki matukio hayo.


Mtuhumiwa huyo wa kwanza kutoka gereza la Guantanamo Bay nchini Cuba alishitakiwa katika mahakama ya kiraia nchini Marekani, ambapo Viongozi wa mashtaka wamesema alihusika kwa asilimia kubwa katika maandalizi na mipango ya kundi la Al Qaeda ya kulipua balozi hizo.


Katika tukio hilo ambapo Watu 224 waliuawa kufuatia mashambulio hayo mawili maafisa wa mahakama walielezea kwamba Ghailani alinunua mitungi ya gesi zilizolipuka pamoja la lori iliyobeba vilipuzi hivyo.


Kwa mujibu wa hukumu hiyo, Mahakama ilimpata Ghailani na hatia moja pekee ya kupanga kuharibu mali na majengo ya serikali ikiwa ni baada ya ushahidi uliokuwa umewasilishwa mbele ya mahakama hiyo kukataliwa kwa sababu zilikusanywa kwa njia isiyo rasmi.(Picha kwa hisani ya mtandao)

No comments:

Post a Comment