Friday, November 19, 2010

Mafunzo yamefanya nizaliwe upya!


SIKU ya kwanza wakati nahudhuria mafunzo haya nilikuwa na dhana tofauti kuhusiana na matumizi ya Internet,kwani nilikuwa nikituma na kupokea E mail, kutuma habari na picha pamoja na matumizi mengine ambayo hayakuwa makubwa.

Mafunzo haya yamenifanya nizaliwe upya kwani,ninaweza kufanya kazi ya uandishi wa habari ambao unakwenda na wakati ikiwa ni pamoja na kuongeza taarifa zingine za kina ambazo ninaweza kuzipata katika Internet kupitia mitandao mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.Mafunzo haya yamekuja kwa wakati muafaka ninaishukuru sana Misa Tan pamoja na wadau wengine kwa kuandaa mafunzo haya.

Thursday, November 18, 2010

Ghailani aingia matatani





MTANZANIA Ahmed Khalfan Ghailani aliyekuwa akikabiliwa mashtaka 281 yakiwemo ya mauaji katika mashambulizi ya kundi la kigaidi la Al Qaeda, dhidi ya ubalozi wa Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998,amepatikana na hatia ya kula njama na kushiriki matukio hayo.


Mtuhumiwa huyo wa kwanza kutoka gereza la Guantanamo Bay nchini Cuba alishitakiwa katika mahakama ya kiraia nchini Marekani, ambapo Viongozi wa mashtaka wamesema alihusika kwa asilimia kubwa katika maandalizi na mipango ya kundi la Al Qaeda ya kulipua balozi hizo.


Katika tukio hilo ambapo Watu 224 waliuawa kufuatia mashambulio hayo mawili maafisa wa mahakama walielezea kwamba Ghailani alinunua mitungi ya gesi zilizolipuka pamoja la lori iliyobeba vilipuzi hivyo.


Kwa mujibu wa hukumu hiyo, Mahakama ilimpata Ghailani na hatia moja pekee ya kupanga kuharibu mali na majengo ya serikali ikiwa ni baada ya ushahidi uliokuwa umewasilishwa mbele ya mahakama hiyo kukataliwa kwa sababu zilikusanywa kwa njia isiyo rasmi.(Picha kwa hisani ya mtandao)

Shirika la Green Belt Movement




UKIZUNGUMZIA suala la uhifadhi na utunzaji wa mazingira,hautakuwa umetenda haki iwapo hutalitaja Shirika la Kimataifa la Green Belt Movement lililoanzishwa nchini Kenya mnamo mwaka 1977 chini ya mwasisi wake, Profesa Wangari Maathai.

Shirika hilo lenye sura mbili,moja ya kimataifa na ile ya kitaifa nchini Kenya limeundwa kama moja ya mashirika ya wanawake ya kiraia, ambalo limelenga katika kutetea haki za binadamu na kusaidia utawala bora na demokrasia ya mabadiliko ya amani kwa njia ya ulinzi wa mazingira duniani kwa ujumla.


Katika taarifa zake kuhusiana na shirika hilo,mwasisi huyo Profesa Maathai amesema lengo la kuundwa kwa shirika hilo ni kuziwezesha jamii duniani kote na kulinda mazingira na kukuza utawala bora na utamaduni wa amani baina ya kizazi kimoja na vijavyo.(Picha kwa hisani ya mtandao wa Green Belt Movement)

Wednesday, November 17, 2010

Day 3

On the third day which was specified for the Eid el Hajj've learned how to put the Blog one another, finding networks internationally, for example BBC Swahili,Mwananchi,Daily News,.Raiamwema.Ippmedia,internetworldstats,print, and get detailed information about the leaders of African countries and the world at large .

Tuesday, November 16, 2010

Day 2

Lesson today I know how to open a Blog, But previously  it was difficult to know what to do in this, Mr Peik Johansson is really knowledgeable in his profession
As a journalist every day I read in some newspapers as a citizen, Guardian, Nation to allow me to get information on the country and internationally, I know this makes me different issues going on in the world.

Mapya kwangu!

Siku ya kwanza ya mafunzo kuhusu masuala ya Internet tuejifunza masuala mengi hususan matumizi ya mtandao katika kumsadia mwandishi wa habari kutafuta na kutuma habari ambazo zimefanyiwa utafiti na taarifa za kutosha.

Waandishi wa habari wanaweza kutumia mtandao katika kutafuta taarifa za kina kwenye Internet ambapo wanaweza kufanya booking hata za tiketi za ndege au treni katika mji wowote dunia, kupata ramani za miji na hata kufahamu hali ya hewa.

Monday, November 15, 2010

Hey karibu Tanzania

My Name is Nakajumo James, I am a Journalist, representing the Swahili newspaper called Habarileo in Kilimanjaro region.

I’m in Arusha for five days attend the workshop organized by Media Institute of Southern Africa, Tanzania Chapter (MISA-TAN) in collaboration with VIKES (Finnish Foundation for Media and Development).